Hopp til hovedinnhold

Bokstart kwa kiswahili

Athari chanya za kusoma hadithi  na watoto 

  • Haijawahi kuwa  mapema sana kusoma kitabu pamoja na watoto. 
  • Hauhitaji kusubiri hadi mtoto wako awe na lugha - kusoma kunawapa lugha! 
  • Kuwasomea hadithi watoto wachanga huwapa hamu ya vitabu na kuimarisha ukuzaji wa lugha. 
  • Wakati wa kusoma huunda mwelekeo wa kawaida na wakati mzuri. 
  • Pamoja mnajenga uhusiano salama na wenye nguvu. 

 

Wakati mtoto ana umri wa miezi 6 
Kusoma kunaweza kuanza kama mchezo! mwachilie mtoto wako achunguze kitabu - akishike, ahisi kurasa na kusigeuza mbele na nyuma. Keti chini pamoja naye kwenye sakafu na kushirikiana kwa mchezo. Ongea kuhusu picha , elekeza kwa kidole ukiyumia sauti. Kwa njia hio, mtoto hugundua kuwa vitabu vinajenga ukaribu, furaha na uzoefu wa pamoja. 


Wakati mtoto ana umri wa mwaka 1
 
Mtoto hupenda kuelekeza kidole kwa picha – elezea kwa maneno kwa kile mnachotazama na kuzungumza pamoja naye. Kusoma kitabu haimaanishi kusoma kutoka mwanzo hadi mwisho, lakini kujiunga na mchezo na kufuatilia hatua za mtoto. 


Wakati mtoto ana umri wa miaka 1.5
 
Mtoto mara nyingi hupenda vitabu vilivyo na hali zinazojulikana kutokana na maisha ya kila siku au picha zilizo na hisia wazi. Kuwa msomaji anayehusika - tumia sauti yako na sura ya uso, na uzungumze kuhusu kile mtoto wako anaitikia. Usiogope kurudia! Kitabu hicho hicho kinaweza kusomwa mara kwa mara, kwa furaha ya mtoto anayekitambua tena. 


Wakati mtoto ana umri wa miaka 2
 
Sasa hapa mnaweza kuanza kusoma vitabu vifupi vya picha pamoja. Chunguza picha, zungumza juu ya kile unachokiona, na umruhusu mtoto ashiriki kwa kusoma. Katika ukaguzi wa miaka 2 kwenye kituo cha afya, utapokea kadi ya zawadi ili kupata kitabu kipya. 


Kusoma vitabu kwa lugha ya kiasili :
 
Lugha ya mama iliyokuzwa vizuri humpatia mtoto msingi bora wa kujifunza lugha zingine. Lugha ya kwanza na lugha ya pili zinasaidiana, kwa hivyo ni muhimu kusoma katika lugha zote mbili. Kwenye maktaba unaweza kuazima vitabu kwa lugha nyingi. 


Matukio katika maktaba
 
Kwenye tovuti yetu unapata habari kuhusu matukio ya shughuli  za mtoto wa miaka 0-2: Bibliotekets arrangementer til de minste — Bergen Offentlige Bibliotek